KLABU ya Galatasaray imemnasa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Wesley Sneijder kwa ada euro milioni 8.3 kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia. Galatasaray yenye maskani yake nchini Uturuki imesema kuwa imesainisha nyota huyo mkataba wenye thamani ya euro milioni kwa mwaka mpaka mwaka 2016 baada ya kushindwa kuafikiana suala la malipo na Inter. Sneijder alijiunga na Inter akitokea Madrid mwaka 2009 na kuisaidia klabu hiyo kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Serie A na Kombe la Italia mwaka 2010. Wakati pazia la usajili wa dirisha dogo likielekea kufungwa Januari 31.
Mamia ya watu wakifurika kumuona Sneijder uwanja wa ndege Ataturk
washa washa !!
Angalia mapaparazi nyuma, wengine kamera, simu na wengine ni furaha tu kumuona live.
Sneijder akikutana na viongozi mbalimbali hapa
Kila mahali ilikuwa ni Sneijder, Sneijder wakilia sahihi yake
No comments:
Post a Comment