TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 22, 2013
MZUNGUKO WA PILI VPL JUMAMOSI, DARAJA LA KWANZA FEB 2
Wakati mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari
22 mwaka huu), mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
umesogezwa mbele kwa wiki moja ambapo sasa utaanza Februari 2 mwaka huu.
Uamuzi wa VPL kuendelea Januari 26 mwaka
huu ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na klabu za ligi hiyo kilichofanyika jana (Januari
21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, uamuzi huo umefikiwa huku
yakiwepo masharti kadhaa kutokana na uamuzi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kukamata sh. milioni 157 kwenye akaunti za TFF, fedha
ambazo zilitoka kwa mdhamini wa VPL (Kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom) kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi hiyo.
Masharti hayo yatawasilishwa na Kamati
ya Ligi kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), nakala kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo. Awali klabu kupitia Kamati ya Ligi zilisisitiza zisingecheza
ligi hadi fedha hizo zitakaporejeshwa.
Kwa upande wa FDL itaanza bila timu ya
Small Kids ya Rukwa ambayo imeshushwa daraja kwa mujibu wa kanuni baada
ya kushindwa kucheza mechi mbili katika mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo,
matokeo yote ya mechi ambazo Small Kids ilicheza katika mzunguko huo wa
kwanza yamefutwa. (Ratiba ya VPL imeambatanishwa).
OCHIENG, AKUFFO WAFIKIA MUAFAKA SIMBA
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za
Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Alex
Mgongolwa imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya klabu ya
Simba lililowasilishwa na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffo
baada ya pande hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji hao kutoka Kenya na Uganda
waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati wakipinga kukatizwa mikataba
yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo, pande zimefikia makubaliano ya
kuvunja mikataba nje ya kamati, na wachezaji hao kulipwa stahili zao.
Pia Simba imekiri kudaiwa na wachezaji
Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor Costa na Rajab Isiaka na kuahidi
kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal Union na mchezaji wake Mohamed
Issa wamefikia makubaliano ya malipo, hivyo kuvunja mkataba kati ya
pande hizo mbili.
SHABANI KADO AIDHINISHWA COASTAL UNION
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za
Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu kupitia maombi ya usajili wa
dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado ameidhinishwa kuidakia timu ya
Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji wengine waliodhinishwa kwenye
dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano ni Humphrey Mieno, Brian Umony,
Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah Seif, Malika Ndeule na Uhuru
Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi, Njaidi Mohamed na Mahmoud Mbulu
(Ruvu Shooting), Mohamed kayi na Emmanuel Gabriel (Tanzania Prisons).
Nurdin Selemani, Shaibu Nayopa, Hamidu
Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses, Muharami Mnyangamala, Majaliwa
Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT), Shukuru Kassim, Chacha Marwa,
Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor Bundala, Delta Thomas, Edward Mzeru
na Tizzo Chomba (Polisi Morogoro), Edmund Kashamila na Julius Mrope
(Kagera Sugar).
Rajab Mohamed, Zakayo Joseph, Baraka
Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar), Zahoro Pazi- kwa mkopo, Emmanuel
Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon Naftali (JKT Ruvu), Moaka
Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi (Mgambo Shooting), Donald
Obimma, Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na Ulugbe Odia (Toto
Africans).
Obadi Mungusa, Juma Seif, Yusuf Mgwao,
Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally- kwa mkopo, Buya Jamwaka, Takang
Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, Athuman
Kajembe na Jarufu Kizombi (African Lyon), Mussa Mudde na Abel Dhaila
(Simba).
Rashid Simba, Zuberi Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na Shabani Kado (Coastal Union).
Mchezaji Martin Mlolere aliyeombewa
usajili Mgambo Shooting kutoka Majimaji amekataliwa kwa vile taratibu za
uhamisho hazijakamilika, hivyo anabaki kwenye timu yake ya Majimaji.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
VODACOM PREMIER LEAGUE: RATIBA:RAUNDI YA PILI
26 JAN 2013 - 18 MEI 2013
Januari 26
African Lyon v Simba [National Stadium, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Polisi Morogoro [Manungu, Morogoro]
Coastal Union v Mgambo JKT [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu Shootings v JKT Ruvu [Mabatini, Pwani]
Azam v Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
JKT Oljoro v Toto Africans [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Januari 27
Yanga v Tanzania Prisons [National Stadium, Dar es Salaam]

No comments:
Post a Comment