BUKOBA SPORTS

Monday, January 21, 2013

OSITA IHEME MCHEZA FILAMU MBILIKIMO WA KINIGERIA ANAYESHINDWA KUCHAGUA MCHUMBA

MSANII mbilikimo wa filamu za Kinigeria, Osita Iheme aliye maarufu kwa jina la Pawpaw au “Ukwa” amejikuta ‘akichanganyikiwa’ katika kuchagua mwanamke wa kuoa miongoni mwa marafiki zake na mashabiki wake wanawake.

Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano na Entertainment Express, Pawpaw alisema kuwa kuchagua mwanamke wa kuoa ni kitu kinachomuumiza kichwa kwa sasa.

“Changamoto ni kwamba sijui ni yupi wa kuoa. Hakika sijachagua, nina marafiki wengi wa kike pamoja na mashabiki.


“Baadhi yao ni wapenzi, lakini kuchagua mtu nitakayeshirikiana nae kwa maisha yangu yote ndicho kitu kinachonifanya nichelewe. Lakini Mungu atanisaidia hivi karibuni, kwa sababu kwake yeye kila kitu kinawezekana,” alisema.

Mshirika wa Pawpaw aliyepata nae umaarufu baada ya kutoka na filamu ya ‘Aki Na Ukwa’ mwaka 2006, Chinedu Ikedieze, anayejulikana zaidi kwa jina la Aki, tayari amefunga ndoa.

No comments:

Post a Comment