TAMASHA kubwa la vipaji litafanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Ikondolelo, iliyopo Kibamba jijini Dar Jumapili hii. Warembo zaidi ya thelathini (30) wataingia katika kuonesha vipaji mbalimbali vikiwemo Kucheza ngoma, Kuimba, pamoja na kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.
Katika Tamasha hilo maalum, Mgeni Rasmi atakuwa Mheshimiwa Idd Azan, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni. Sambamba na hayo mheshimiwa Azan atazindua tuzo mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo zengine mbalimbali.
Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000 , Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000.
Tamasha litaanza kuanzia sa nane mchana na kuendelea.
Asante.
Fredy Tony Njeje
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano
No comments:
Post a Comment