BUKOBA SPORTS

Monday, January 28, 2013

VODACOM PREMIER LEAGUE: YANGA YAIFUNGA PRISON MABAO 3-1, YAENDELEA KUSHIKILIA USUKANI


wachezaji wa Yanga wakishangilia

Timu ya Yanga imeifunga Prison ya Mbeya mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi unaliochezwa uwanja wa Taifa.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Jerry Tegete kipindi cha kwanza na lingine kipindi cha pili na tatu limefungwa na Mbuyi Twite kipindi cha pili.
Lile la Prison lilifungwa na Elias Maguri baada ya kuwazidi mbio mabeki na kufanikiwa kusawazisha bao.

Mapema kabla ya mchezo kiungo wa Yanga, Frank Domayo alipatwa aliugua ghafla na jina lake kutolewa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake ikachukuliwa na Nurdin Bakari na Prison ilipata pigo pale mshambuliaji mpya Emmanuel Gabriel alipoenguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Elias Maguri, kwa sababu ya kutokuwa na leseni ya TFF ya kumruhusu kucheza Ligi Kuu.
Kikosi cha Yanga; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Nurdin Bakari, Didier Kavumbangu, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.

TZ Prisons; David Abdallah, Aziz Sibo, Henry Mwalugala, Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Nurdin Issa, Sino Augustino, Freddy Chudu, Elias Maguri, Misango Magai na Jeremiah Juma.

No comments:

Post a Comment