BUKOBA SPORTS

Tuesday, February 12, 2013

KOCHA STEVEN KESHI AONDOA WASIWASI, SASA KUENDELEA NA NIGERIA

KOCHA wa timu ya taifa ya Nigeria, Steven Keshi ataendelea kuifundisha timu hiyo baada ya waziri wa michezo wa nchi hiyo Bolani Abdullahi kufanya mazungumzo ya kina na kocha huyo. Mgogoro uliopo kati ya Keshi na Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF lilipelekea kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 kutangaza kujiuzulu katika kituo cha redio cha Metro FM nchini Afrika Kusini. Lakini mara baada ya waziri huyo kufanya nayemazungumzo jana jijini Johannesburg alifanikiwa kumshawishi kocha huyo kuendelea na kibarua chake ingawa haikufafanuliwa kwa undani mazungumzo yao yalihusiana na nini. Pia kuna taarifa kuwa mazungumzo ya usuluhishi kati ya Keshi na NFF yataendelea wakati timu hiyo itakapowasili jijini Abuja baadae leo.

No comments:

Post a Comment