MANCHESTER, England
Mtaliano huyo anaamini nafasi ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu itakuwa kubwa, kama kikosi hicho cha Alex Ferguson kitasonga mbele katika michuano hiyo kwa kuiondoa Real Madrid na kutinga robo fainali
ROBERTO Mancini anayeinoa Manchester City, ameshangaza mashabiki wa soka kwa kusema yu tayari kubeba bendera ya rangi nyekundu na nyeupe kuwashangilia mahasimu Manchester United katika mechi yao dhidi ya Real Madrid, wiki ijayo.
Mtaliano huyo aliyeipa ubingwa wa England Manchester City ana matumaini kwamba vinara na mahasimu wao Man United watafanya vema katika pambano la mtoano wa 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya kikosi cha Jose Jose Mourinho.
Mancini anaamini nafasi ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu itakuwa kubwa, kama kikosi hicho cha Alex Ferguson kitasonga mbele katika michuano hiyo.
Lakini dua ya Mancini anaomba wakati akiwatambua vema miamba hiyo ya soka la Hispania na Ulaya kwa ujumla, baada ya kuwa alicheza na kikosi hicho mara mbili katika hatua ya makundi ya michuano hii msimu huu.
Na yeye licha ya kusema atawaunga mkono, lakini amekiri kuwa United inahitaji msaada wote inaohitaji kuweza kupata matokeo mazuri dhidi ya Madrid.
Alipoulizwa kama angependa kuona Man United ikiichapa Madrid, Mancini alisema: “Ndiyo, itakuwa mechi mbili nyingine dhidi yao. Nitakwenda huko na kuwaunga mkono nikiwa na bendera nyeupe na nyekundu ya United.
“Lakini kucheza na Madrid ni ngumu mno, wao ni moja ya timu bora kabisa duniani kwa sasa. Wao pamoja na mahasimu wao Barca. Wana wachezaji wazuri, lakini pia historia ya kuvutia. Itakuwa ngumu mno kwa United kuwafunga Madrid, kwa sababu klabu yao iko juu.”
Akizungumzia pengo la pointi alilonalo dhidi ya vinara Man United, Mancini alisemma: “Kama tuliweza kutwaa ubingwa msimu uliopita ambao walikuwa kileleni kwa point nane mechi sita kabla ya kumaliza msimu, iweje tushindwe mwaka huu kukiwa na mechi 14 kumaliza ligi?”

No comments:
Post a Comment