
KLABU PEKEE ya Tanzania ambayo bado imo
kwenye Michuano ya Klabu Barani Afrika, Azam FC, leo imeanza vyema Mechi
yake ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya Kombe la Shirikisho
kwa kuifunga Barrack Young Controllers II Bao 2-1 huko Mjini Monrovia,
Liberia.
Hadi Mapumziko Azam FC walikuwa nyuma
kwa Bao 1-0 lakini Kipindi cha Pili waligangamala na kupiga Bao mbili
Wafungaji wakiwa Humphrey Mieno, Mchezaji kutoka Kenya, na Bao la
ushindi kupatikana Dakika ya 90 Mfungaji akiwa Seif Abdallah Karihe
kufuatia kazi njema ya Khamis Mcha ‘Vialli.’
Azam FC na Barrack Young Controllers II watarudiana Jijini Dar es Salaam kwenye Wikiendi ya kuanzia Aprili 6.
Mshindi wa Mechi hiyo atasonga Raundi ya
Mtoano ya Timu 16 na watakaofuzu hatua hiyo wataingia hatua ya Makundi
itayochezwa Mtindo wa Ligi.
Kufuatia kubwagwa nje ya Michuano ya CAF
ya CHAMPIONS LIGI kwa Simba na Jamhuri ya Zanzibar, Azam FC ndie
Mwakilishi pekee Barani Afrika.
KIKOSI CHA AZAM FC KILICHOANZA
Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Ibrahim Mwaipopo, Humphrey Mieno, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’, John Bocco, Kipre Tcheche
No comments:
Post a Comment