BUKOBA SPORTS

Monday, March 18, 2013

RAIKKONEN WA LOTUS AIBUKA BINGWA KATIKA MASHINDANO YA AUSTRALIA GRAND PRIX. AWABWAGA CHINI FERNANDO ALONSO NA SEBASTIAN VETTEL!!

Triumphant: Kimi Raikkonen celebrates after winning the first race of the seasonDEREVA wa Lotus, Kimi Raikkonen amefanikiwa kuibuka kidedea katika mashindano ya Australia Grand Prix baada ya kufanikiwa kumpita Fernando Alonso wa timu ya Ferrari. Katika mashindano hayo ambayo jana yaliahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Melbourne, Raikkonen alisimama mara mbili kubadilisha matairi yake ukilinganisha na mpinzani wake wa karibu Alonso ambaye alisimama mara tatu na kutumia mwanya huo kushinda. Bingwa wa Dunia mwaka jana Sebastian Vettel wa Red Bull alishika nafasi ya tatu mbele ya Felipe Massa wa Ferrari na Lewis Hamilton wa Marcedes. Nafasi ya sita katika mbio hizo ilikwenda kwa Mark Webber wa Red Bull akifuatiwa na Adrian Sutil na Paul di Resta kutoka timu ya Force India ambao walishika nafasi ya saba na nane wakati nafasi ya tisa ilikwenda kwa Jenson Button wa MacLaren na kumi bora ilifungwa na Romain Grosjean wa Lotus.

1-2-3: Raikkonen (katikati) akishangilia akiwa na Fernando Alonso (kushoto) na mshindi wa tatu kulia Sebastian Vettel
Kama kawaida yetu baada ya kushinda lazima tumimine..

Raikkonen akiendesha kwa spidi kali

Sebastian Vettel na Raikkonen wakipeana vituz

Podium fun
Lewis Hamilton akispata nafasi ya tano akiendesha Mercedespatashika hapa kwenye Albert Park circuit

Kwenye Ukodak wa pamoja hapa baada ya kumaliza mizunguko yao

No comments:

Post a Comment