BUKOBA SPORTS

Saturday, April 6, 2013

ASKOFU MPYA WA BUKOBA MHASHAMU ASKOFU DESIDERIUS RWOMA KUSIMIKWA KESHO JUMAPILI.

Askofu Desiderius Rwoma alizaliwa mwaka 1947 katika parokia ya rutabo, Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba. Parokia moja na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa.







Alipata upadrisho kwa mikono ya Baba Askofu Nestor Timaywa, mwaka 1974 pale Rutabo.

· Akiwa jimboni Bukoba aliwahi kuwa gambera (Mkuu wa shule) ya seminari ya Rubya kwa miaka mingi. Wakati wake shule ya Rubya mara kadhaa ilikuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani na karibu mara zote ilikuwa kila mara kati ya shule 10 bora taifani. Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo anawajua vizuri na wanampenda.

· Vile vile alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la masista wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila mara amekuwa karibu nao.

· Kabla ya kuteuliwa kuwa askofu wa singida alikuwa makamu wa askofu na hivyo kulijua jimbbo la Bukoba na uongozi wake. Alifanya kazi hii vizuri sana na hivyo kuteuliwa kuwa askofu wa Singida.
Akiwa askofu wa Singida (1999 – 2013) ameonyesha karama zake za uongozi. Ameweza kuleta maendeleo ya kichungaji na kibinadamu katika jimbo. Ameonnyesha uelewano wake kwa kuwaalika mashirika mengi ya kitawa ambayo kila moja limeleta karama yake ya maendeleo, uchungaji, shule, vituo vya afya, maendeleo ya akina mama na vijana nk.

· Katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasimamia idara kubwa ya Utume wa walei
Askofu Desiderius Rwoma ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda maendeleo. Ana uhusiano mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia, kabila, taifa au dini.


WANABUKOBA NA WANAKAGERA WANAKUKARIBISHA KWA FURAHA NA SHANGWE, KARIBU NYUMBANI




Askofu Desiderius Rwoma ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda maendeleo. Ana uhusiano mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia, kabila, taifa au dini.

No comments:

Post a Comment