BUKOBA SPORTS

Saturday, April 6, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: READING 0 vs SOUTHAMPTON 2. KOCHA NIGEL ADKINS AANZA KWA KICHAPO CHA NYUMBANI

Wakicheza Ugenini Southampton leo waimebuka na ushindi wa alama 3 muhimu kwa kuwafunga bao 2-0 wenyeji Reading wanaoongozwa na kocha mpya. Magoli ya Southampton zimepatikana dakika ya 34 kipindi cha kwanza kupitia mchezaji Jay Rodriguez wakati la pili likifungwa kipindi cha pili na mchezaji Adam Lallana. Ushindi huu unawaweka Southampton nafasi ya 11 na pointi 37 huku Reading wakibaki mkiani na alama zao 23 na timu zote mbili zikibakiza michezo 6 msimu kuisha.  Jay Rodriguez akiteleza na kufunga bao la kwanza kwa timu yake ya Southampton leo mchana

Kilio ugenini: kipa na mchezaji wa Reading wakiwa hoi..baada ya kutupiwa bao la 2
Kocha Nigel Adkins (kulia) akisisitiza mashambulizi, kumbuka kocha huyu alitimuliwa katika timu hii ya Southampton kabla  ya kutua hapa Reading hivyo vijana hawa wa Southampton anawajua..

Hapa kazi tu: Chris Gunter akichuana na Rodriguez
Adam Lallana akishangilia baada ya kuziona nyavu kwa bao la pili dakika ya 72

VIKOSI:
Reading: Federici, Kelly, Mariappa, Morrison, Gunter, Robson-Kanu (Hunt 73), Karacan, Guthrie (McCleary 62), Akpan (Leigertwood 46), McAnuff, Le Fondre.
Subs: McCarthy, Pearce, Pogrebnyak, Harte.

Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Shaw, Ramirez (Lallana 63), Schneiderlin, Cork, Steven Davis (Do Prado 89), Rodriguez, Lambert.
Subs: Kelvin Davis, Fonte, Fox, Ward-Prowse, Puncheon.
Goals: Rodriguez 35, Lallana 72.
Ref: Mike Jones.

No comments:

Post a Comment