BUKOBA SPORTS

Monday, April 8, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: MANCHESTER UNITED 1 vs MANCHESTER CITY 2, CITY WAIFUKUZIA UNITED KILELENI!!

Timu zote mbili zimeanza kwa kukamiana sana kila timu ikitaka kumfunga mwenzake.Timu ya City ikifanya mashambulizi zaidi ya United. Dakika ya 29 mchezaji wa Manchester City David Silva akaunawampira kwa kujificha na mwamuzi Mike Dean akamwona na kumpa kadi ya njano.
Dakika ya 42 Vicenty Kompany akamfanyia ndivyo sivyo Ashley Young na kupewa nae kadi ya njano. kipindi cha pili kuingia dakika ya 51 mchezaji wa City Milner akaipatia bao City baada ya Ryan Giggs kurudisha mpira nyuma kwa pasi hewa.  Dakika ya 59 mchezaji Phill Jones anaipatia bao Manchester United na kusawazisha baada ya Rvp kupiga frii kiki hadi golini. Patashika inatokea kati ya Jones kupiga kichwa na mpira unamgonga Kompany kuishilia nyavuni na kuwa 1-1. Dakika ya 78 United wakazidiwa nguvu na mchezaji kutoka benchi Aguero na hatimaye  akawachoma bao la pili na kufanya 1-2 dhidi ya United, bukobasports.com yashuhudia mtanange huo usiku huu.

Kocha wa City Mancini na kocha wa United Ferguson wakisalimiana kabla ya mtanange usiku huu.
Welbeck akiachia shuti kali kujaribu kufunga

Mchezaji wa United Patrice Evra akipiga mpira kwa kichwa juu James Milner to a header

Van Persie akiachia shuti kali na hatimaye mchezaji Kompany kuzuia shuti hiloVan Persie na Kompany wakichuana vikali uwanjani old Trafford usiku huu.
Milner na Ryan Giggs kwenye patashika

Hapa hupiti hata ukizunguka....mchezaji wa City Tevez akiwa amezungukwa na wachezaji wa United

Kompany akionekana kwenye picha na refa Dean baada ya kupewa kadi ya njano

Wachezaji wa City wakimpongeza Milner

Wachezaji wa City wakimpongeza Milner baada ya kufunga bao la pili.

Kipa wa City Hart akidaka hewa baada ya frii kiki ya Van Persie na Kompany kujifunga

Mchezaji Jones aliyesababisha bao la United kupatikana baada Kompany kujifunga akishangilia

Kazi kweli kweli...Tumejifunga...
Kimbiza kimbiza ya Aguero ikazaa bao...

Fantastc finish ...Aguero akishangilia bao lake la pili na la ushindi.
Mashabiki wa United wakiwa wamebeba bango lao(banner) kabla ya mtanange huo.

VIKOSI:
Man United: De Gea; Rafael, Ferdinand, Jones, Evra; Carrick, Giggs; Young (Kagawa 90+2), Rooney (Hernandez 85), Welbeck (Valencia 80); Van Persie.
Subs not used: Lindegaard, Nani, Cleverley, Buttner.
Booked: Rooney, Rafael, Valencia.
Goal: Kompany (OG) 59.
Man City: Hart; Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy; Y Toure, Barry; Milner, Silva (Lescott 89), Nasri (Aguero 71); Tevez (Javi Garcia 90+4).
Subs not used: Pantilimon, K Toure, Kolarov, Dzeko.
Booked: Silva, Kompany, Tevez, Barry, Zabaleta.
Goals: Milner 51, Aguero 78.
Referee: Mike Dean. 


MSIMAMO ULIVYO KWA SASA TIMU 5 ZA JUU
2012-2013 Barclays Premier League Table
Overall
Home
Away
POS
TEAMPWDLFA
WDLFA
WDLFA
GDPts
1 Manchester United 31 25 2 4 71 33
14 0 2 40 17
11 2 2 31 16
38 77
2 Manchester City 31 19 8 4 57 27
11 3 1 35 11
8 5 3 22 16
30 65
3 Chelsea 31 17 7 7 61 33
10 4 2 35 13
7 3 5 26 20
28 58
4 Tottenham Hotspur 32 17 7 8 55 40
8 5 3 24 17
9 2 5 31 23
15 58
5 Arsenal 31 16 8 7 61 34
9 3 3 39 20
7 5 4 22 14
27 56

MECHI 3 ZA MANCHESTER UNITED ZIJAZO 

Tarehe 14.4. 2013  - Stoke (A) Prem
            17.4.2013   - West Ham (A)  Prem
            22.4.2013   - Aston Villa (H)  Prem



MECHI 3 ZA MANCHESTER CITY ZIJAZO
Tarehe  14.4.2013  Chelsea (A)  FAC
             15.4.2013 West Brom (H) Prem (Umehairishwa)
             17.4.2013 Wigan (H)  Prem

No comments:

Post a Comment