BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 9, 2013

UHURU KENYATTA AAPISHWA LEO KUWA RAIS RASMI WA KENYA.


Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapishwa hii leo na kuchukua uongozi kutoka kwa Rais Mwai Kibaki.
Hii ni baada ya Uhuru kumshinda Raila Odinga katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe nne mwezi Machi
.Wageni mashuhuri wakiweno marais wa nchi kadhaa za Afrika pamoja na wanadiplomasia na maelfu ya wananchi walishuhudia sherehe hizo katika uwanja wa michezo wa Kasarani viungani mwa mji wa Nairobi.
Rais mpya wa Kenya Odinga hakuhudhuria sherehe hizo baada ya jitihada zake kutaka mahakama ya juu zaidi kubatilisha matokeo ya uchaguzi kukosa kufua dafu.
Tukio hilo ni kilele cha uchaguzi wa Machi 4 uliofanyika kwa amani ambapo Kenyata alimshinda Waziri Mkuu anayaeondoka madarakani Raila Odinga . Rais huyo ameahidi kufanya kazi kuboresha maisha ya Wakenya wote.

Viongozi wengine wengi barani Afrika walihudhuria hafla hiyo, ikiwa ni pamoja viongozi wa mataifa ya nchi jirani za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Baadhi ya mataifa ya magharibi yaliwakilishwa na mabalozi wao wakati wakijaribu kupunguza mawasiliano na rais huyo kutokana na kesi inayomkabili huko ICC.

Wakati wa hotuba katika sherehe za kuapishwa rais wa Uganda Yoweri Museveni aliwapongeza Wakenya kwa kumchagua Bw.Kenyatta na akikaidi kile alichosema kuwa ni kurubuniwa na ICC.

Rais Kenyatta anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa shutuma za kusaidia ghasia za baada ya uchaguzi mapema 2008 ambazo zilipelekea vifo vya watu zaidi ya 1,100 na wengine 600,000 kupoteza makazi yao. Kesi yake itaanza kusikilizwa mwezi Julai.

Kenyatta na naibu wake William Ruto wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC . Wanadaiwa kuwa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika miaka mitano iliyopita.
Wakati huo wawili hao walikuwa mahasimu wa kisiasa na wote wanakanusha madai dhidi yao.

No comments:

Post a Comment