BUKOBA SPORTS

Sunday, April 7, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: TOTTENHAM 2 vs EVERTON 2, BAO LA GYLFI SIGURDSSON LAWAOKOA DAKIKA ZA LALA SALAMA.


Huko White Hart Lane, Bao la Gylfi Sigurdsson limewaokoa Tottenham na kuwapa sare ya Bao 2-2 walipokutana na Everton. Spurs ndio waliotangulia kufunga Bao Sekunde 33 tangu Mpira uanze baada ya Emmanuel Adebayor kukwamisha wavuni krosi ya Jan Vertonghen. Lakini Everton wakasawazisha kupitia Phil Jagielka na kufunga Bao lao la pili na la kuongoza kupitia Kevin Mirallas.Droo hii ya timu hizi inairudisha Spurs katika nafasi ya nne wakiwa na alama 58 sawa na Chelsea wenye alama 58 waliofunga leo Sunderland bao 2-1 na wakitofautiana mabao ya kufunga. Huku Everon wakiwa nafasi ya 6 wakiwa na pointi 52 juu ya Arsenal wenye pointi 56.
Wachezaji wa zamani Paul Gascoigne na Gary Mabbutt wakicheki mtanange huo.Emmanuel Adebayor akifurahia baada ya kuipatia bao timu yake dakika ya 1
Kumbuka: Bao la Adebayor ni la pili kwa kufungwa mapema katika Ligi Kuu na Tottenham na la kwanza ni lile la Mchezaji wao Ledley King aliefunga Sekunde 10 toka Mpira uanze walipocheza na Bradford Desemba 2000.
Victor Anichebe wa Everton, Hugo Lloris wa Tottenham Hotspur na Steven Caulker wa Tottenham Hotspur wakiangalia mpira ukitupwa nyavuni na Emmanuel Adebayor goli la kwanza na dakika ya 1Jan Vertonghen wa Tottenham Hotspur akimtoa mpira Victor Anichebe wa EvertonClint Dempsey akiachia shuti kali ambalo limepanguliwa na  Darron GibsonKevin Mirallas akiwafungia bao la pili Everton Dakika ya 53Scott Parker akichuana na mchezaji wa  Everton Nikica JelavicGylfi Sigurdsson wa Tottenham Hotspur akisawazisha bao dakika ya 87
Gylfi Sigurdsson wa Tottenham Hotspur kifurahia bao lake la dakika za lala salama.


RATIBA/MATOKEO
Jumapili 7 April
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Liverpool 0 v West Ham 0

[Saa 10 Dak 5 Jioni]
Tottenham 2 v Everton 2
[Saa 11 Jioni]
Chelsea 2 v Sunderland 1
Newcastle 1Vv Fulham 0
[Saa 12 Dak 10 Jioni]
QPR 1 v Wigan 1

Kesho Jumatatu 8 Aprili
[Saa 4 Usiku]
Man United v Man City

No comments:

Post a Comment