BUKOBA SPORTS

Saturday, April 6, 2013

GUARDIOLA KUINOA RASMI BAYERN JULAI 14.

KOCHA mpya wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola anatarajiwa kuanza kusimama rasmi katika benchi la ufundi la klabu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Hansa Rostock Julai 14 mwaka huu. Guardiola mwenye umri wa miaka 42 alichukua likizo ya mwaka mmoja baada ya kuondoka katika klabu ya Barcelona ya Hispania mwishoni mwa msimu wa 2011-2012 lakini Januari mwaka huu Bayern walimtangaza kocha huyo kama mbadala wa kocha wa sasa Jupp Heynckes mwishoni mwa msimu huu. Bayern watacheza mchezo wa kirafiki na Hansa ambao wako katika ligi daraja la tatu ili kuwasaidia kupata fedha za kulipa madeni makubwa yanayoikabili klabu hiyo ndogo. Mara baada ya mchezo huo wa kirafiki siku 10 baadae Guardiola atakuwa katika Uwanja wa Allianz Arena kuikaribisha timu yake ya zamani ya Barcelona katika mechi nyingine ya kirafiki.

No comments:

Post a Comment