BUKOBA SPORTS

Friday, May 31, 2013

KIFO CHA NGWEA: LADY JAYDEE NAYE ASITISHA SHOW YAKE, ILIKUWA IFANYIKE LEO HII IJUMAA!!!

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, mwanadada Judith Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa kufariki nchini Afrika Kusini jana.

Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kutitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.

Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi sana kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na kukabwa na kilio.


HII HAPA PICHA YA MWILI WA MAREHEMU ALBERT NGWEA UKIWA MOCHWARI


Tumelazimika kuweka picha hii kutokana na maombi ya mashabiki wake ambao hawatapata nafasi ya kumuaga msanii huyu na kutoa salamu zao za mwisho.....

R.I.P NGWEA

No comments:

Post a Comment