ENGLAND imetoka sare ya 1-1 na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kirafiki usiku jana kwenye Uwanja wa Wembley. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa William Collum wa Scotland, Ireland ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao ugenini, mfungaji Shane Long dakika ya 13, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Seamus Coleman kutoka wingi ya kulia.
Frank Lampard aliwasawazishia wenyeji dakika 10 baadaye, yaani dakika ya 23 kuftaia kazi nzuri ya Daniel Sturridge ambaye aliambaa uipande wa kushoto wa box, kabla ya kummiminia krosi mfungaji, aliyemtungua kipa Glenn Whelan.
Ashley Cole alipewa kofia ya dhahabu baada ya kutimiza mechi 100 za timu ya taifa ya England jana usiku.
Alex Oxlade-Chamberlain akipigana vikali na mchezaji wa Ireland jana usiku
Nivute nikuvute...
James Milner na Alex Oxlade-Chamberlain wakijiandaa kucheza mpira uliopigwa juu
Bao la kichwa likiingia nyavuni na Ireland kujipatia bao la kuongoza na kufanya 1-0 dhidi ya England
Haikupita muda Frank Lampardaliwasawazishia England bao na kufanya 1-1
Theo Walcott akishangaa shangaa jana usiku
Kikosi cha England: Hart/Foster dk46, Johnson/Jones dk46, Cahill, Jagielka, Cole/Baines dkl54, Walcott, Lampard, Carrick, Oxlade-Chamberlain/Milner dk 87, Rooney na Sturridge/Defoe dk 33.
Ireland: Forde, Coleman, O'Shea, St. Ledger, Kelly, Walters/Sammon dk82, McCarthy, Whelan/Hendrick dk74, McGeady/McClean dk68, Long na Keane/Cox dk 66.
No comments:
Post a Comment