BUKOBA SPORTS

Friday, May 17, 2013

MAMBO YANAZIDI KUNOGA .... DULLY SYKES KUPAMBA USIKU WA REDD'S MISS MOSHI 2013 AVENTURE KESHO JUMAMOSI.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Dully Sykes "mista Misifa" anatarajia kupanda jukwaani kutumbuiza katika usiku wa Ulimbwende, usiku wa Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika May 18, katika ukumbi wa Aventure, Mjini Moshi.
Akizungumza mratibu wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa kampuni ya New Vision plan inayohusika na kazi za kuandaa mashindano ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya warembo19 watachuana kumsaka malkia wa Moshi wakisindikizwa na Prince Dully Sykes.

Moses alisema tayari maandalizi yameshaanza na mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote wameshaingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.

FAINALI za kumsaka Redds Miss Moshi 2013 itakayofanyika kesho, mwaka huu katika ukumbi wa Aventure uliopo Moshi
Akizungumza kwa njia ya simu, mratibu wa mashindano hayo, Moses Komba alisema kuwa jumla ya walibwende wapatao 19 watachuana kumsaka malkia wa Moshi.
Moses alisema tayari mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote waliingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.

“Maandalizi yamekamilika na warembo wote wapo kambini katika ukumbi wa Aventure na tunategemea wadau watashuhudia kitu tofauti katika shindano la mwaka huu,” alisema Komba. Pia alisema viingilio katika mashindano ya mwaka huu, viti vya dhahabu viingilio vitakuwa sh. 50,000, viti vya V.I.P vitakuwa ni sh. 30,000 na viingilio vya kawaida ni sh. 15,000.

Wadhamini wengine na Redds, Panone, Baba G na Zoom Net Printers ambapo kwa upande wa burudani alisema atakuwepo msanii mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine kutoka Moshi.

No comments:

Post a Comment