BUKOBA SPORTS

Saturday, May 18, 2013

MSAFARA WA MAGARI UNAOPITA MIKOA MBALIMBALI KUTOA ELIMU KUHUSU FISTULA WAZINDULIWA BUKOBA

Balozi wa vodacom Mwana FA akimsikiriza mgeni rasmi mkuu wa wilaya bukoba mama zippola pangani muda mfupi kabla ya kumpa funguo za gari ndogo tax itakayo zunguka maeneo yote yaliyopangwa kutoa elimu kuhusa fistula inatibika.

Umati wa watu ukisikiliza elimu kuhusu fistula, ugonjwa unaowapata akina mama wakati wa kujifungua


Ni shirika lisilo la serikali ambalo linawataalamu wakiwemo madakitari, kampuni ya vodacom imewakabidhi kiasi cha shilingi bilioni nane kusaidia kutibu wakina mama wenye fistula shirika hili hutoa huduma za matibabu bure zikiwemo na gharama usafiri,chakula na malazi,baada ya wataalamu kubaini tatizo lafistula
Katibu tawala wa mkoa wa kagera(kushoto) akikaribishwa eneo la tukio soko kuu bukoba

Meneja mahusiano ya nje vodacom salumu mwalimu akitoa maelezo kwa nini vodacom imeamua kusaidia akina mama katika janga hili la fistula,kikubwa alisema vodacom kile inachokipata inajari sana huduma za jamii,na aliwataka wamama wanapopata vistura wasikate tamaa ya maisha vodacom kazi ni kwako
Balozi wa vodacom mwana FA akisikiliza kwa makini




Bi Naima ishengoma mkazi wa katoro bukoba vijijini akitoa ushuhuda ,baada ya kupata fistula mwanaume alimkimbia,lakini kupitia redio karagwe alipata habari na alipelekwa CCBRT na sasa amepona,aliwasisitiza wamama ambao fistula wasikate tamaa unatibika, tena huduma bure
Shuhuda sofia ibrahimu wa kyerwa karagwe,pamoja na ushuhuda mwingi aliotoa alimshukuru mume wake amidu winstoni kwa kumvumilia kipindi chote cha ugonjwa bila kumnyanyapaa,kumtenga,na kumuhudumia mpaka sasa kapona
Katibu tawala mkoa wa kagera akimkaribisha mgeni rasmi azungumze

Mgeni rasmi mkuu wa wilaya bukoba akitoa neno kwenye uzinduzi wa msafara kupita mikoa mbalimbali kutoa elimu kuhusu fistula inatibika
Piga hiyo namba ni bure eleza tatizo lako la fistula utasaidiwa
Gari maalumu linotumika katika msafara, Lakini kwa mimi binafsi nimejiuliza maswali mengi sana mbona simuoni Mwanadada Lady Jay Dee ...Komandoooo!
Balozi wa vodacom mwana FA kwa heshima ya wakazi wa bukoba alimwaga mistari


Dj slay kwa siku hiyo alikuwa mc wa shughuli nzima,hapo yupo na balozi wa vodacom mwana FA

Ulifika wakati wa mgeni rasmi kukabidhi ufunguo kuashiria uzinduzi wa msafara

Mr. Jamal Kalumuna akiwa na balozi wa vodacom mwana FA


MENEJA MAHUSIANO YA NJE VODACOM AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KABLA YA MSAFARA KUONDOKA KUPITIA ,CHATO,GEITA, MWANZA , SHINYANGA,SINGIDA,MOROGORO NA ATIMAE TAREHE 23-5-2013 MSAFARA UTAPOKELEWA NA MH RAIS JAKAYA KIKWETE,PONGEZI VODACOM NA CCBRT KWA KUONYESHA UZALENDO KWA AKINA MAMA

No comments:

Post a Comment