BUKOBA SPORTS

Saturday, May 18, 2013

NAY WA MITEGO NA DIAMOND PLATINUMZ BIFU TUPU LEO DARLIVE!!! TAYARI WAMEANZA KTUPIANA VIJEMBE VYA NGUVU MTAANI, DAR LIVE LEO KUAMUA NANI ZAIDI!!!!

Baada ya mechi ya Simba na Yanga leo Taifa jioni magari yote ya abiria yatanyoosha njia kuelekea Dar live kupeleka wadau kushuhudia Nay wa Mitego na Diamond Platinumz wakichuana vikali, huku wote wakiwa wamepandwa na jaziba na maneno ya Vijembe ambavyo kila mmoja wao yamemfanya apandwe na hasira pamoja na jeuri ya kupambana jukwaani kuoneshana kazi wazi wazi mbele ya mashabiki, huku Nay akijisimamia na Hip Hop na Diamond Platinumz mzee wa kubana pua akisimamia Bongo Flava. Wadau na Wapenzi wao watakao ingia Dar live ndiyo watakao chagua na zaidi kati ya Hip Hop na Bongo Flava. Hivyo mnaombwa kuja kwa wingi Dar Live kujionea mtanange huo wa kukata na shoka huku wakizindua hiyo video ya MUZIKI GANI inayotamba karibu Nchi nzima na Africa Mashariki inayowalaza wao wenyewe milango wazi kila kukicha!!!!! huku wote wakiwa wametoka vifua wazi kama Mabaunsa!!Nay ''Napenda kumwambia bwana mdogo Diamond kuwa leo akae tayari kwa kuwa naenda kuandika historia Mpya Darlive, Nataka watanzania wote wajitokeze waje kuona navyomkalisha mbana pua na wavaa nguo za dada zao wanaojidai kwenda sawa na utandawazi......''Nay alizidi kufunguka kuwa leo ndo utakuwa mwisho wa Diamond na kumthibiishia kuwa Hip Hop ndo muziki unaolipa na wenye maana zaidi......!!
Diamond Platinumz.
Diamond mwenyewe ameiambia bukobasports.com kuwa amejipanga kisawasawa kuonesha ujuzi wake leo ndani ya Dar Live leo usiku saa 1:00 hadi Majogoo, Bongo Flava na Hip Hop tutaoneshana ni ipi itaibuka juu, Mashabiki mtanionea wazi..Patashimbika leo mpaka kielewe!!!

No comments:

Post a Comment