BUKOBA SPORTS

Saturday, May 18, 2013

VODACOM TANZANIA PREMIER LEAGUE: SIMBA 0 v YANGA 2, KAVUMBAGU NA KIIZA WACHINJA MNYAMA LEO TAIFA!!

Mabingwa wapya Yanga leo wamewapa raha Mashabiki wao kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo baada ya kuwabwagiza mabao 2-0 Simba na kumaliza msimu wao vizuri wa msimu huu 2012-2013 kwa aina hiyo ya Shangwe zaidi.
Yanga wanaifunga Simba kwa mara ya 24 wakiwazidi zaidi watani zao hao huku wao Simba wakiwa wameifunga Yanga mara 19 tu, Ila mpaka sasa Mnyama Simba anaongoza kwa kuifunga mabao mengi zaidi Yanga rekodi ambayo bado hawajaivunja mpaka sasa, Pia leo wakionekana kupunguza magoli hayo ambayo mpaka mara ya mwisho walifungwa mabao 5-0.
Mbwembwe za wanayanga..Barabarani..!!Wpenzi wa Yanga na wadau wakiingia uwanjani leo mchanaWasanii JB na Ray wakiteta jambo baada ya kukuta getini hapaingiliki kiurahisi kwa sababu ya wingi wa watu ambao walikuwa mpaka muda wa saa 9 mchana walikuwa wengi nje ya uwanja wakipanga foleni.Baadaye walipata nafasi ya kuingia kwenye lango jingineHao wanaingia....Ngoja niingie ili nikuletee matukio zaidi ya ndani....Usibanduke hapa!!.
MATUKIO YA MTANAGE MZIMA YANAFATA PUNDE!!! KARIBU BUKOBASPORTS.COM

No comments:

Post a Comment