BUKOBA SPORTS

Sunday, June 9, 2013

TAIFA STARS YAPIGWA 2-1 NA MOROCCO NA KUIWEKA HATARINI NAFASI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014

Matumaini ya Tanzania kushiriki michuano ya kombe la dunia yameanza kupotea baada ya leo hii kufungwa na Morocco kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kugombania nafasi ya kwenda Brazil 2014.

Mchezo huo uliofanyika Morocco, Stars walimaliza mechi wakiwa pungufu baada ya Aggrey Morris kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza baada ya kumchezea madhambi Abderazak Hemed hivyo kupelekea Morocco kupata penati iliyowapa bao la kuongoza.
Kipindi cha pili Morocco wakaongeza bao la pili dakika ya 50 kupitia Youssef El Arabi kabla ya Amri Kiemba kufunga bao la Stars dakika 10 baadaye. 
Kutokana na matokeo haya Stars wanabaki nafasi ya pili kwa pointi 6 nyuma ya Ivory Coast wanaongoza kwa pointi 10 huku kumebakiwa na michezo miwili miwili katika kundi A linalojumuisha pia timu ya Gambia.
Stars wamebakiwa na mechi dhidi ya Ivory Coast itakayopigwa taifa na Gambia itakayopigwa ugenini.

wadau
Kikosi cha Stars
Juma Kaseja (1) capt, Aggrey Morris (6), Patrick Kelvin Yondani (5), Domayo Frank Raymond (16) Ngassa Mrisho Alfani (8), Erasto Nyoni (4), Salum Salum Abubakar (2), Ulimwengu Thomas Emmanuel (11), Shomari Kapombe (20), Mbwana Samattah (10), Ramadhani Amri (9).

Wachezaji wa Akiba ni
Mwadini Ali (18) Juma Vicent (19), Ali Nurdin Haroub (13), Athumani Idd (3), Mwitula Mwinyi (15), Abbas Mudathiri (17), Khamis Mcha (7), Msuva Simon (12), Chanongo Haruni (21), BocoJohn (14), Shabani Pazzi Zahoro (22), Mtinge Ally Mustafa (23)

Wakati Taifa stars ikifungwa, wenzao Ivory coast imeshinda mabao 3-0 dhidi ya Gambia, mabao ya Ivory coast yamefungwa na Lasina Traure dakika ya 12, Wilferd Bony dakika ya 62 na Yaya Toure dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo Ivory coast inaongoza kundi ikiwa na pointi 10, Tanzania pointi 6, Morocco pointi 5 na Gambia wanabaki na ponti yao 1. 


Hadi mapumziko:
Morocco 1 - 0 Tanzania

Dakika ya 52
Morocco 2 - 0 Tanzania

Dakika ya 62
Morocco 2 - 1 Tanzania

Dakika ya 80
Morocco 2 - 1 Tanzania

FULL TIME
Morocco 2 - 1 Tanzania

No comments:

Post a Comment