Bangkok, Wednesday 17 July, 8.00pm local time
Rajamangala Stadium
Meneja mpya wa Manchester United David Moyes amestushwa na mapokezi makubwa waliyopata walipotua Bangkok, Thailand Siku ya Alhamisi ikiwa ni hatua ya kwanza ya Ziara yao.
Alisema: “Umati wa Watu waliokuwepo Uwanja wa Ndege unashangaza na ile shamrashamra ni kama Beatles wametua…Ni kitu cha ajabu. Wapo Mashabiki nje na ndani ya Hoteli yetu na kila tunapokwenda. Hii inaonyesha nguvu ya Man United. Sijui kama ntaizoea hali hii!”
Moyes afurahishwa na kusaka Wapya, Adai hawajasema Alcantara yumo!
Jose Mourinho, Frank Lampard, Eden Hazard wakiwasili mjini Bangkok
Mashabiki wa Chelsea wakiwa wamebeba picha ya the special one "Jose" huko Thailand
JOSE Mourinho amekiri kuwa ni shabiki wa Wayne Rooney, lakini David Moyes akamjibu haraka kuwa “Wayne Rooney hatauzwa.” Chelsea imewasili leo Bangkok huko Thailand kuelekea maandalizi yao ya msimu mpya, wakati staa huyo wa Manchester United akirudishwa nyumbani England. Mshambuliaji huyo wa England pia alikuwa Bangkok na klabu yake ya United, lakini amerudishwa nyumbani kutokana na kusumbuliwa na misuli ya paja, hali inayomuweka nje ya mwanzo wa msimu mpya. Rooney amekuwa akihusishwa kuhamia Stamford Bridge kiangazi hiki baada ya Alex Ferguson kudai kuwa alitaka kuondoka United

Jose akitupa tano zake kwa wadau!!
Kuhusu Thiago Alcantara kukaribia kusainiwa na Bayern Munich kutoka Barcelona wakati imevumishwa Man United inamtaka na ni mmoja wa walengwa wao, Moyes alijibu: “Sikusema hilo!”
Pia alifafanua: “Wapo Wachezaji tunaowalenga hivi sasa. Kwa wakati huu, tuna furaha na jinsi vitu vinavyokwenda.”
Pia Moyes alipuuza swali kuhusu kauli ya Jose Mourinho kuwa anampenda Wayne Rooney na kujibu: “Watu wanaruhusiwa kuwa na maoni yao kuhusu Wachezaji wazuri. Nina hakika Jose ameulizwa kuhusu Wachezaji wengi. Nitarudia tena: Wayne Rooney ni Mchezaji wa Manchester United na atabaki kuwa hivyo”
Kuhusu kuumia kwa Rooney, Moyes alisema wao imebidi wachukue tahadhari na sasa inawezekana akawa nje kwa Wiki mbili au tatu tu na atakuwa huko Manchester akifanya Mazoezi kwenye Jimu na Bwawa la Kuogelea.
Rooney alirudishwa Manchester mara tu baada ya kutua huko Bangkok, Thailand baada kuwa na maumivu ya Musuli ya Pajani.
Jana Rooney alitoa Posti kwenye Ukurasa wake wa Facebook akisikitika kwa kupata maumivu Mazoezini lakini anategemea si kitu cha kutisha sana.
No comments:
Post a Comment