Hadi Dakika 90 kumalizika matokeo yalikuwa Ghana 2 Chile 2.
Ghana walipata Bao la kwanza katika Dakika ya 11 baada ya Frank Acheampong kumtengenezea Moses Odjer alieweka kifuani na kuachia shuti kali lakini Chile walijibu kwa Bao 2 za haraka za Nicolas Castillo na Mchezaji wa Manchester United Angelo Henriquez kwenye Dakika za 23 na 27.
Ghana walifanya Gemu kuwa 2-2 katika Dakika ya 72 kwa Bao la Ebenezer Assifuah na Mechi kuingia Dakika za Nyongeza 30.
Katika Dakika ya 98, Angelo Henriquez aliipeleka Chile kuwa 3-2 lakini Seidu Salifu akaisawazishia Ghana katika Dakika ya 113 na Assifuah kuipa ushindi kwa Bao la 4 katika Dakika ya 120.
MAGOLI:
Ghana 4
-Dakika ya 21 Odjer
-72 & 120 Assifuah
-113 Salifu
Chile 3
- Dakika ya 23 Nicolas Castillo
-27 & 98 Angelo Henriquez
Katika Robo Fainali iliyotangulia Jana
Usiku, Iraq mara 3 waliongoza lakini mara zote South Korea walisawazisha
kwenye Mechi ambayo ilimalizika Bao 2-2 katika Dakika 90 na kuongezwa
Dakika za Nyongeza 30.
Katika Dakika hizo za Nyongeza, Iraq
walifunga Bao lao la 3 katika Dakika ya 118 lakini katika Dakika ya
mwisho ya muda wa majeruhi, South Korea walisawazisha katika Dakika ya
122 na ndipo ikaja Tombola ya Mikwaju ya Penati ambazo Iraq walishinda
kwa Penati 5-4 wakati South Korea walipokosa Penati 2 na Iraq 1.
MAGOLI:
Iraq 3
-Dakika ya 21 Atiyah Ali Faez
-42 & 118 Farhan
South Korea 3
- Dakika ya 25 Kwon Chang Hoon
-50 Lee Joo-Young
-122 Jung
Nusu Fainali zitachezwa hapo Jumatano Julai 10 kwa France kucheza na Ghana kisha kufuatia Iraq v Uruguay.
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
45 06/07 France 4 Uzbekistan 0
46 06/07 Uruguay 1 Spain 0
47 07/07 Iraq 3 South Korea 3 [Dak 120 3-3, Iraq Washindi Penati 5-4]
48 07/07 Ghana 2 Chile 2 [Dakika 120, Ghana 4 Chile 3]
NUSU FAINALI
49 10/07 18:00 Bursa France v Ghana
50 10/07 21:00 Trabzon Iraq v Uruguay
MSHINDI WA TATU
51 13/07 18:00 Istanbul L49 v L50
No comments:
Post a Comment