Veterani huyo ameondoka Fulham kama Mchezaji huru baada ya kuikataa Ofa ya Klabu hiyo ya kumpa Mkataba mpya na sasa yupo Stamford Bridge kuleta upinzani kwa Kipa Nambari Wani Petr Cech.
Schwarzer ndie Mchezaji wa kwanza kutoka nje ya Uingereza kucheza Mechi 500 za Ligi Kuu England.

Veterani huyo, aliezaliwa huko Sydney, Australia, alihamia England Mwaka 1996 na kujiunga na Bradford City na kisha Middlesbrough alipoicheza Mechi zaidi ya 400 katika Miaka 11 na Mwaka 2008 kujiunga na Fulham. Huyu ni Mchezaji wa tatu kusajiliwa na Kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho, katika Kipindi hiki na wengine ni Marco van Ginkel toka Holland na Mchezaji wa Kimataifa wa Germany Andre Schurrle.
No comments:
Post a Comment