GHANA, Wawakilishi pekee wa Afrika waliobakia GHANA, Jana Usiku walitupwa nje ya MASHINDANO Ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Vijana chini ya Miaka 20, U-20, walipotolewa kwenye Nusu Fainali iliyochezwa huko Nchini Turkey kwa kufungwa Bao 2-1na France.
France sasa itacheza Fainali na Uruguay ambayo iliitoa Iraq kwa Penati 7-6 baada ya kutoka Sare ya Bao 1-1 katika Nusu Fainali nyingine iliyochezwa huko Turkey hiyo Jana kwenye Mechi iliyomalizika 1-1 katika Dakika 90 na kubaki 1-1 hadi Dakika 120 zilipomalizika na ndipo Tombola ya Mikwaju ya Penati kuipa ushindi Uruguay.
FRANCE 2 vs GHANA
Huko Bursa Ataturk Stadyumu, Mjini Bursa, Jana France ilitinga Fainali kwa kuilaza Ghana Bao 2-1 na hii ni mara ya pili kwa France na Ghana kukutana kwenye Mashindano haya huko Turkey.
Awali, kwenye Mechi ya Kundi lao, France iliipiga Ghana Bao 3-1.
Kwenye Nusu Fainali ya Jana, France walitangulia kufunga kwa Bao la Thauvin lakini Dakika 4 baadae Mfungaji hatari wa Ghana, Assifuah, alisawazisha.
Hadi Mapumziko, Bao zilikuwa 1-1.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 74, Thauvin tena akaifungia France Bao la Pili na la ushindi.
No comments:
Post a Comment