wadau wakifatilia kabumbu kwa hali ya juu sana na makini
Wachezaji wa Miembeni wakishangilia kwa kurudi kati
Wakati mtananange unaendelea kwenye jukwaa la Balimi palikuwa hapatoshi mashabiki baadhi walikuwa wanatupiana makonde
Patashika za hapa na pale kwenye jukwaa la Balimi!!!!!!!!!
Wachezaji wa Miembeni wakishangilia baada ya kutupia nyavuni na kufanya 2-0
Miembeni wakishangilia wachezaji
Rwamishenye nao wakafunga bao na kufanya 2-1 kipindi cha pili
...Zamu yetu sasa na sisi tushangilie!!
Baadaye kidogo Rwamishenye wakafunga bao la kusawazisha la utata na kufanya 2-2
Wakati kocha anapuliza kipenga cha kumaliza mechi, Wachezaji wa timu ya Rwamishenye walifunga bao jingine la utata tena na kumfanya refa ababaike tena huku wachezaji wakimlalamikia kuwa bao la haki!!!
Refa alimaliza mechi kama hivi na huku lawama zikimwandama hadi nje ya uwanja !!
Mashabiki wakiandamana nje ya uwanja kujua kuwa lipi na lipi ni 2-2 au ni 3-2, swali hili lilipata msemaji wake ambaye ni Refali wa mchezo huo kwa kudai kuwa mtanange huu ni sare ya 2-2.
Mashabiki wakijiuliza yaliyotokea uwanjani jioni hii kati ya Miembeni na Rwamishenye
Siyo kweli!!! ongea ukweli ....hapa kuna namna!!! ni Kamala akiteta na kiongozi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja!
No comments:
Post a Comment