BUKOBA SPORTS

Wednesday, July 10, 2013

WACHEZAJI WA MACHESTER UNITED WAPAA KUELEKEA BANGKOK

DAVID MOYES ametaja Kikosi cha Wachezaji 19 wa Manchester United ambao leo wataruka kuelekea Bangkok, Thailand, ikiwa ni hatua ya kwanza ya Ziara yao ya huko Bara la Asia ni miongoni mwao wapo Wayne Rooney na Wilfried Zaha. 
Katika Ziara hiyo, ambayo itawachukua Nchi za Thailand, Australia, Japan na Hong Kong, Mastaa watatu, Robin van Persie, David De Gea na Shinji Kagawa, hawamo lakini wataungana na wenzao baadae.
Robin van Persie na David De Gea watajumuika na wenzao huko Sydney, Australia na Shinji Kagawa atawasubiri wenzake huko huko kwao Japan ambako yuko kwa likizo.
Makocha wapya nao ndani Ryan Giggs na Phil Neville, wakiwa wanaoneshana ujumbe kwenye simu muda mchache kabla ya kupaa na ndege kuelekea Bangkok.

KIKOSI KAMILI:

MAKIPA: Anders Lindegaard, Ben Amos
MABEKI: Rafael, Phil Jones, Rio Ferdinand, Jonny Evans, Patrice Evra, Alex Büttner, Fabio, Michael Keane
VIUNGO: Michael Carrick, Anderson, Tom Cleverley, Ryan Giggs, Wilfried Zaha, Jesse Lingard, Adnan Januzaj
MASTRAIKA: Wayne Rooney, Danny Welbeck


RATIBA MAN UNITED KABLA MSIMU MPYA KUANZA:
July 13 Singha All Star XI (Rajamangala Stadium, Bangkok - Singha 80th Anniversary Cup) 2pm
July 20 A-League All Stars (ANZ, Stadium, Sydney) 10.30am
July 23 Yokohama F-Marinos (Nissan Stadium, Yokohama) 11.20am
July 26 Cerezo Osaka (Osaka Nagai Stadium, Osaka) 11am
July 29 Kitchee (Hong Kong Stadium, Hong Kong) 1pm

No comments:

Post a Comment