




Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akitoa hotuba kwa wanamichezo kutoka wizara, idara za serikali baada ya mazoezi makali asubuhi Jumamosi, Agosti 24, 2013 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Balozi Sefue aliyekuwa mgeni rasmi, awali aliongoza maelfu ya wanamichezo hao kukimbia umbali wa kilomite 3 na kufuatiwa na mazoezi ya kunyoosha viungo yaliyofanyika uwanja wa Taifa. Mashindano ya SHIMIWI mwak 2013, yatafanyika mkoani Dodoma ambapo michezo zaidi ya 20 kushindaniwa chini ya udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akijikunjua wakati wa mazoezi hayo

Washiriki wakifanya mazoezi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Agosti 24, 2013

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akiwapasha habari waandishi siku ya Jumamosi Agosti 24, 2013, juu ya udhamini wa mfuko huo kwenye mashindano ya mwaka huu ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), wakati wa uzinduzi uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wanamichezo walikimbia umbali wa kilomita 3 na kufanya mazoezi ya kukata na shoka yaliyoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, LuluMengele. na Watatu kushoto ni Afisa Masoko wa PPF, Seleki
No comments:
Post a Comment