BUKOBA SPORTS

Thursday, August 29, 2013

MESEN SELEKTA AMEANZA KUSAKA VIPAJI VYA WANAWAKE WENYE TALENT YA UIMBAJI.


Mtayarishaji anayechipukia katika muziki wa Bongo flava Jerry Boniface aka Mesen Selekta ameanza kuwatafuta wanawake wenye vipaji vya uimbaji.

Baada ya kujinyakulia tuzo ya Kili kwa mtayarishaji bora anayechipukia, kwa sasa producer wa De fetality Music, Mesen ameanza mchakato wa kuwatafuta wanawake wenye vipaji vya uimbaji ili kuingia katika label.

Mesen Selekta aliongea na mwandishi wa BK Magazine na kusema” Actualy Mesen Selekta kupitia De fatality Music tumeona kuanza kuvisaka vipaji vya wanawake wanaojua kuimba ili waweze kuingia label, fursa hii ipo wazi kwa Wanawake kuanzia sasa waje wafanye usahili.”

No comments:

Post a Comment