BUKOBA SPORTS

Thursday, September 5, 2013

BOSI CRYSTAL PALACE IAN HOLLOWAY AFUNGIWA MECHI 2!

Meneja wa Crystal Palace Ian Holloway amefungiwa Mechi mbili kwa Kosa la Utovu wa Nidhamu kufuatia kuwabwatukia Marefa mara baada ya Timu yake kufungwa Bao 1-0 na Tottenham hapo Agosti 18.
Pia, Holloway amepigwa Faini ya Jumla ya Pauni 18,000.
Katika Mechi hiyo, Crystal Palace walifungwa kwa Bao la Penati iliyotolewa na Refa Mark Clattenburg na kufungwa na Roberto Soldado.

FA imesema Hollowaya atazikosa Mechi za Ligi za Old Trafford Crystal Palace itakapocheza na Man United hapo September 14 na Wikiendi inayofuata Mechi ya Nyumbani na Swansea City.


Pamoja na Mechi hizo, Holloway amepigwa Faini ya Pauni 10,000 kwa Lugha na Matendo yake dhidi ya Marefa wa Mechi husika na Pauni 8,000 kwa Matamshi yake baada ya Mechi hiyo.

Baada ya Mechi hiyo, Holloway alitamka: “Huu utakuwa Msimu mrefu kwangu kwa ajili ya Watu hawa [Marefa]. Nilipata hili nikiwa Blackpool. Kuna Klabu zinapewa Faulo na nyingine hazipewi!”

No comments:

Post a Comment