Wawili hao walitoa mkwanja huo mwezi uliopita kama na walikuwa wakitakiwa kuhudhuria mahakamani kwenye kesi mnamo September 17, ingawa wakili wao aliomba keshi hiyo iharishwe kwa sababu walikuwa na majukumu mengine siku hiyo.
Mchezaji huyo bora wa dunia na baba yake, wote waligoma kufanya makosa hayo, walituhumiwa kuficha zaidi euro millioni 4 wakati walipopeleka taarifa zao za mapato yao katika miaka ya 2006 mpaka 2009.
Uuzwaji wa haki za taswira ya Messi umekuwa ukifichwa kwa kutumia mtandao fulani katika nchi za Uruguay, Belize, Switzerland na United Kingdom, mwendesha mashtaka ya jinai huko Catalonia alisema.
'Sijawahi kuhusika na suala kama hili hata baba yangu pia,' Messi alisema mwezi July.
'Tuna mawakili wetu na watu wanaosimamia rasilimali zetu na tunawaamini watasimamia hili na kulimaliza.' - Messi
Messi amekuwa mkazi wa Barcelona tangu 2000 na tayari amepata uraia wa Hispania tangu 2005.
Anatengeneza kaisi cha £13 million kupitia matangazo ya kibiashara yakiwemo makampuni kama Adidas, PepsiCo, P&G na Turkish Airlines, pia anaingiza kiasi cha £13million kwa msimu kupitia maishahara na bonasi - na yupo katika top 10 ya wanamichezo wanaoingiza fedha nyingi kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment