BUKOBA SPORTS

Saturday, September 7, 2013

COSTA RICA YAILAZA MAREKANI BAO 3-1 MICHUANO YA CONCAF


Timu ya Costa Rica imefifisha mbio za Marekani kuelekea katika kombe la dunia mwaka 2014 kwa kuipa kichapo cha magoli 3-1 jana Ijumaa, wakati Mexico imeshuhudia mzizimo wa hali ya juu baada ya kupoteza nafasi kwa kuchapwa magoli 2-1 na Honduras.
Costa Rica imesogea katika nafasi ya juu kwenye kundi la mataifa sita yaliyofuzu michuano hiyo ya CONCAF ikiibuka na ushindi huko San Jose kwenye mtanange uliotamatisha mechi ya 12 ushindi mwembamba wa Marekani.


Timu hiyo kwa sasa inaongoza kundi hilo kwa alama 14 , ikiizidi timu ya taifa ya Marekani kwa alama moja. Mexico, ambao wamekuwa vinara wa muda mrefu katika kanda hiyo, wako katika hali mbaya zaidi wakati wakielekea katika duru nyingine muhimu ya mechi ya Jumanne.
Hapa hupiti!!

Bao!! Clint Dempsey akishangilia baada ya kufunga mkwaju wa penati

Kwenye patashika hapa!..
Mchezaji wa Costa Rica akishangilia  Clint Dempsey...Hoi!! Mchezaji Landon Donovan akiachia shuti kali hapa wakati wanacheza na Costa Rica Kipa wa Marekani Brad Guzan akidaka shuti lililopigwa na mchezaji wa Costa Rica.

No comments:

Post a Comment