BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 10, 2013

DK. SHEIN CUP: KITAMLI YA NUNGWI YAIBABIZA MWENDO MDUNDO YA KIDOTI BAO 1-0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi Kipa Bora wa mashindano ya ujirani mwema ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Nungwi.
Balozi Seif akimkabidhi Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi Makame Mohd Haji jezi na vifaa baada ya timu hiyo kuibuka bingwa wa Dr. Sheni Cup huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja
Balozi Seif akimkabidhi Kikombe Kepteni ya Mabanati wa Timu ya Pete ya Tusitengane ya Nungwi Ndamu Makame Mussa baada ya kuibuka na ushindi wa Kombe la Mwanamwema Sheni dhidi ya Timu ya Pete ya Tuko Imara.

Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi Makame Mohd Haji akifuahia kikombe anachokabidhiwa na mgeni rasmi balozi Seif baada ya kutawadhwa kuwa mabingwa wa kombe hilo.
Kati kati yao ni lezi wa Jimbo la Nungwi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa wa Idara Maalum Haji Omar Kheir.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Michezo Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar katyika kubadilishana mawazo ya namna ya kufufua michezo ya ndani inayoonekana mingi kufifia.

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Michezo Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis akipokea mchango wa shilingi Milioni 2,000,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kusaidia ufufuaji wa michezo ya ndani inayoonekana kufifia hapa Nchini. Picha na Hassan Issa wa – OPMR – ZNZ.


NA Othman Khamis Ame, OMPR
Hatimae Mabingwa wa Mashindano ya Ujirani mwema ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Nungwi na kufadhiliwa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Sheni amepatikana katika mchezo wa Fainali ya mashindano hayo yaliyozikutanisha Timu za Soka za Kitamli ya Nungwi dhidi ya wapinzani wao Timu ya Soka ya Mwendo Mdundo ya Kidoti.

Pambano hilo la Fainali lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wapenzi wa soka wa Jimbo la Nungwi na Vitongoji vyake limeiwezesha Wenyeji wa mashindano hayo Timu ya Kitamli ya Nungwi kuibuka na ushindi kwa kuilaza Mwendo Mdundo ya Kidoti Goli 1-0.


Timu ya Kitamli ilijipatia goli lake la pekee na la ushindi lililofungwa na mchezaji Haji Wa Haji katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambapo mgeni rasmi katika pambano hilo la Fainali ya Dr. Sheni Cup alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mashindano hayo ya ujirani mwema yaliyoanza kutimua vumbi Tarehe 24/8/2013 yamejumuisha Timu Tisa kutoka katika vijiji tofauti vya Jimbo la Nungwi yakienda sambamba na yale ya mchezo wa Pete { Net Ball } kwa Wanawake yaliyojumuisha Timu Nne.

No comments:

Post a Comment