BUKOBA SPORTS

Saturday, September 28, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: LIVE MATCH- TOTTENHAM 1 v CHELSEA 1, Full time!

Tottenham Hotspurs wakicheza kwao White Hart Lane Mchezaji Gylfi Sigurdsson ndiye aliyeanza kufunga bao dakika ya 20 baada ya kukatiza kwenye  ngome ya Chelsea na kupewa pasi safi na Soldado na hatimaye kuachia shuti mpaka ndani ya lango la Chelsea. Kipindi cha Pili dakika ya 65 John Terry ameisawazishia timu yake bao na kufanya 1-1 baada ya kupigwa Frii kiki na Mata na kisha Terry kuunganisha mpira huo kwa kichwa safi hadi nyavuni.
Wamekutana: Mameneja Andre Villas-Boas na Jose Mourinho, kocha wa Spurs akisalimiana na kocha wa Chelsea Jose Mourinho muda mfupi kabla ya mtanange.Kocha Roy Hodgson nae alikuwepo kuucheki  mtanange huoGylfi Sigurdsson (kushoto) akishangilia baada ya kufunga bao dakika ya 20 mchana huu

Mguu wa kulia ulipiga mpira ukazuiliwa akaumalizia kwa mguu wa kushoto.Wachezaji wa Spurs wakimpongeza mwenzao baada ya kuwapatia bao  Jan Vertonghen akimfanyia ndivyo sivyo  Fernando Torres lakini hakuna kadi iliyotolewa hapoTorres kabla ya kutolewa nje
Mbali ya upinzani ndani ya Uwanja ambapo Tottenham wapo Nafasi ya Pili, Pointi sawa na Vinara Arsenal, na Chelsea wako Nafasi ya 4, Pointi 2 nyuma ya TottenhamHuendi kokote! hapa wachezaji wa Spurs wakimuweka mtu kati hapa..!  Kapteini John Terry akisawazisha bao dakika ya 65
John Terry (kushoto) akishangilia 
Chelsea wanasawazisha bao baada ya kupata frii kiki na Mata akapiga na kisha john Terry akaumalizia kwa kichwa mpaka nyavuni dakika 65 kipindi cha pili.Moussa Dembele akichuana na mchezaji wa Chelsea Eden HazardAndros na Frank LampardAndre Villas-Boas na Jose Mourinho (kushoto) wakioneshana kaziFernando Torres unamfanya nini Jan Vertonghen??
Dakika ya 81 Torres anaondolewa nje kwa kupewa kadi ya njano na kadi nyekundu kwa kumfanyia mchezaji wa Spurs ndivyo sivyo. Dakika 90 zimemalizika Spurs na Chelsea wakitoshana nguvu ya bao 1-1 licha ya Chelsea kucheza pungufu kwa dakika kama 10. Ushindi huu unawapandisha juu kileleni kwa muda Spurs kwa pointi 13 na Chelsea wanapanda juu kidogo kwa alama moja kwa kufikisha pointi 11.Jose Mourinho akimpa maelekezo Juan MataJohn Terry akishangilia bao lake
VIKOSI:
Tottenham: Lloris; Walker, Naughton, Dawson, Vertonghen; Paulinho, Dembele, Townsend (Chadli 63), Eriksen (Holtby 69), Sigurdsson; Soldado (Defoe 76).
Subs: Friedel, Chirches, Lamela, Sandro.
Booked: Townsend, Eriksen, Vertonghen, Dawson, Dembele.
Goal: Sigurdsson 20.
Chelsea: Cech; Ivanovic, Luiz, Terry, Cole; Mikel (Mata 46), Lampard; Ramires, Oscar (Azpilicueta 83), Hazard (Schurrle 69); Torres.

Subs: Schwarzer, Cahill, Essien, Eto'o.
Booked: Torres, Ivanovic.
Sent off: Torres.
Goal: Terry 65.
Ref: Mike Dean.

No comments:

Post a Comment