Washiriki wa shindano hilo wa Dar es salaam wa mwaka jana. Picha na Missie Popular
Mchakato wa kutafuta Washiriki wa Kambi ya Tanzania Top Model ulioanza wiki mbili zilizopita unaendelea mwishoni mwa wiki hii hapa jijini Arusha na Mjini Moshi.Wasichana 20 watakaochaguliwa kutoka maeneo mbalimbali nchini ndio watakaounda kambi ya Taifa ambayo itaendeshwa kama Tamthilia halisi kwenye kituo kimojawapo cha Televisheni ambacho hakijatangazwa. Leo Jumamosi katika ukumbi wa Mango Tree
, Warembo wapatao 25 wako kwenye mchuano mkali wa kuwania nafasi mojawapo kati ya hizo ili waweze kuwakilisha jiji la Arusha kwenye Top Model yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka katika jiji la Dar es salaam. Habari kwa Hisani ya Globu ya Jamii Issa Michuzi
No comments:
Post a Comment