MILAN, Italia
HATIMAYE klabu ya AC Milan imetangaza kupitia mtandao wake kwamba imefanikiwa kumrudisha nyumbani kiungo wake wa zamani, Ricardo Kaka (31), kutoka Real Madrid na imemsainisha mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka San Siro hadi 2015.
Baada ya mazungumzo marefu asubuhi ya jana jijini Madrid, kati ya Adriano Galliani na wawakilishi wa Kaka, walikubaliana Mbrazil huyo ataingiza kiasi cha euro milioni 4 kwa msimu, Kaka anarudi kwenye timu aliyoichezea kati ya mwaka 2003 – 2009.
No comments:
Post a Comment