Di Canio alikorofishana na Refa wa Mechi hiyo Martin Atkinson wakati alipokuwa akilalamikia mbinu za Arsenal za kupoteza muda na Refa huyo akamtoa nje Meneja huyo.
Mwenyewe Di Canio, baada ya Mechi, alieleza: “Nilimwambia Refa kwamba kama unataka kukamilisha kazi yako vizuri nitoe nje! Na Refa hakufanya mzaha, akanitoa!”
Mapema kwenye Mechi hiyo Refa Atkinson aliwaudhi Sunderland pale alipokataa Bao lao safi alilofunga Jozy Altidore kwa madai alifanyiwa madhambi kabla kufunga.
No comments:
Post a Comment