Monday, September 16, 2013

YOHAN CABAYE AOMBA RADHI MASHABIKI NEWCASTLE

KIUNGO wa Newcastle Yohan Cabaye amewataka radhi Mashabiki wa Timu hiyo kwa kugoma kuichezea Mechi Timu hiyo Mwezi uliopita.
Cabaye, Miaka 27, aliikosa Mechi Newcastle waliyotoka 0-0 na West Ham baada ya kugomewa Uhamisho kwenda Arsenal ambao walikuwa wametoa Ofa ya Pauni Milioni 10 kumnunua.

Hivi sasa Cabaye amerudi Kikosini na Jumamosi iliyopita alicheza tangu mwanzo wakati Newcastle inaichapa Aston Villa Bao 2-1 kwenye Ligi.
Yohan Cabaye alijiunga na Newcastle kutoka Klabu ya Ufaransa Lille Mwezi Juni Mwaka 2011.
Cabaye amezungumza: “Kama Mashabiki bado wamekasirika kwa yaliyotokea, naelewa na nawaomba radhi. Nataka tusahau yaliyopita.”

Wakati wa sakata hilo la kutaka kuhama, Cabaye alizikosa Mechi ya ufunguzi wa Msimu wa Ligi na Man City waliyofungwa 4-0 na pia ile ya Capital One Cup walipoifunga Morecambe 2-0 lakini alicheza Mechi na Fulham akitokea Benchi na kushinda 1-0.

No comments:

Post a Comment