BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 3, 2013

MANCHESTER CITY NAO WAFANIKIWA KUSAINI JEMBE MARTIN DEMICHELIS KUTOKA ATLETICO MADRID

MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City imethibitisha kunasa saini ya beki wa kati wa Atletico Madrid, Martin Demichelis (32) kwa dau la pauni milioni 3.5 na kumpa mkataba wa miaka miwili.

Demichelis ametua City ili kuongeza nguvu kwenye beki ya timu hiyo na usajili wake unaifanya Man City kutumia zaidi ya pauni milioni 100 wakati huu wa usajili, baada ya kuwanasa mastaa wengine kama kina Fernandinho, Jesus Navas, Alvaro Negredo na Stevan Jovetic wakati huu Manuel Pellegrini akijipanga kutengeneza timu yake.

No comments:

Post a Comment