Na. Mwandishi wetu.
Kampuni
ya Afrisoft Technologies Ltd inayojihusisha na masuala ya teknolojia
zinazorahisisha maisha ya kila siku, sasa imekuja na huduma mpya ya ‘M-Soka’ ambapo mtumiaji wa mtandao wa Vodacom anaweza kufaidi huduma hiyo kwa muda wowote na kwa haraka zaidi.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni
hiyo Brian Godwin Mushi amesema wameamua kutengeneza huduma hiyo, kwa
kuwa mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana na watu wengi na hivyo
ukizingatia mahitaji ya watu kutaka kujua matokeo au kujua ratiba, sasa
haina haja tena kusubiri gazeti au redio ila ukiingia katika ‘M-Soka’ (Mobile Soka)unapata kila kitu moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi.
Bw.
Mushi amesema ukizingatia hali halisi sio kila mahali panapatikana
huduma ya intaneti na sio kila mtu ana simu inayoweza kuunganishwa
kwenye mtandao huo, hivyo kupitia ‘M-Soka’ unaweza kupata matokeo au
ratiba kwa kutumia simu ya aina yeyote ile.
Akitaja namba zinazotumika kupata matokeo hayo amesema kuwa ni *149*31# kwa gharama nafuu ya shilingi 40 tu.
Amesema
unaweza kupata matokeo ya mechi zilizochezwa, ratiba ya mechi
zitakazofuata na pia msimamo wa ligi mbalimbali, na kuwa kama ni matokeo
unaweza kupata ya leo, jana, juzi na siku moja kabla na kama ni ratiba
utapata ya leo, kesho, keshokutwa na mtondogoo na kama ni msimamo
unapata wa wakati huohuo(real Time).
Pia
kuna ‘option ya live’ ambayo inakuwezesha kufuatilia mpira kwa dakika
hiyo hiyo hata goli likifungwa inakupa matokeo yake mpaka jina la
mfungaji na dakika ambayo goli limefungwa.
Ni
njia rahisi kwa mashabiki kufuatilia matokeo ya timu yao wanayoipenda na
kupata taarifa ya kila kitu ikiwemo magoli, kadi hata penati.
Ligi
zinazopatikana katika mtandao huo ni za Uingereza, Hispania, Ufaransa,
Italia, Ujerumani, UEFA, Kombe la Dunia na CAF kwa shilingi 40 tu.
Kwa mshabiki yeyote wa soka usipate tabu, chukua simu yako na uandike *149*31# na upate matokeo, ratiba na msimamo papo hapo bila shaka na kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment