KLABU ya AC Milan imetangaza katika mtandao wake kuwa kiungo wake nyota Kaka atakuwa nje ya uwanja kwa muda baada kupata matatizo ya msuli katika mchezo dhidi ya Torino mwishoni mwa wiki iliyopita. Kiungo huyo alilazimika kutoka nje ya uwanja baada ya kucheza kwa dakika 70 katika mechi yake ya kwanza toka arejee katika klabu hiyo na kufanyiwa vipimo zaidi na kuthibitisha ukubwa wa tatizo lake. Madaktari wa Milan wataendelea kumfanyia vipimo zaidi nyota huyo kwa siku 10 kabla ya kutaja tarehe rasmi atakayoweza kurejea tena uwanjani. Mapema Kaka amesema alizungumza na viongozi wa Milan na kuweka wazi kuwa hatakuwa akichukua mshahara wake kama atakuwa hachezi kutokana na kuwa majeruhi atakachohitaji yeye ni klabu kumsaidia katika kipindi hicho ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida. Kwasasa Milan inakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi akiwemo Giampaolo Pazzini, Daniele Bonera, M’Baye Niang, Riccardo Montolivo, Mattia De Sciglio, Ignazio Abate na Stephan El Shaarawy.
No comments:
Post a Comment