TANZANIA YAJIKONGOJA YAINGIZA TIMU MBILI TU ROBO FAINALI AIRTEL RISING STARS
Timu zote za wavulana na wasichana zimeingia robo fainali katika michuano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanayofanyika Lagos , nchini Nigeria na mshindi atapata medali , kombe pamoja na dola za marekani 10,000. Timu ya wasichana imetinga robo fainali baada ya ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Malawi jana na kumaliza na pointi nne katika kundi ambapo timu ya Uganda ikishika uskani kwa point sita. Wakicheza kwa kujiami timu ya wasichana ya Tanzania ilipata goli katika dakika ya 17 kupitia kwa mshambuliaji hatari Shelda Boniface, kabla ya Malawi kusawazisha dakika ya 7 kipindi cha pili.
...
No comments:
Post a Comment