BUKOBA SPORTS

Friday, September 6, 2013

ZANZIBAR GRAND MALT PREMIER LEAGUE YAANZA JANA!

>>LEO PEMBA: JAMHURI v KIZIMBANI, UNGUJA: MALINDI v POLISI!!

Pazia la Ligi Kuu Soka Visiwani Zanzibar (ZANZIBAR GRAND MALT PREMIER LEAGUE), limefunguliwa rasmi Jana kwa michezo miwili iliyochezwa katika Viwanja viwili tofauti.

Huko Gombani Kisiwani Pemba Timu ya Jamhuri kutoka Chake Chake waliumana na Timu ngeni katika Ligi hiyo, Fufuni, ambapo pambano hilo lilimalizika kwa Fufuni kuianza vyema Ligi hiyo kwa ushindi wa Bao 1-0.
Bao la Fufuni lilipatikana katika dakika ya 25 likifungwa na Ramadhan Sultan.

Kwa upande wa Kisiwani Unguja nako kulikuwa na mchezo mmoja uliowakutanisha Makamo Bingwa wa Msimu uliopita Timu ya Chuoni wakikabiliana na Mafunzo katika Uwanja wa Mao Tse Tung, ambapo pambano hilo lilimalizika kwa Mafunzo kuianza vyema Ligi hiyo baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Mafunzo yote mawili yakifungwa na Abdulrahman Abdallah katika dakika ya 29 na 85, na bao pekee la Chuoni likifungwa na Abdulkadir Ibrahim katika dakika ya 67.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena hii leo kwa michezo miwili, wakati Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani itawashuhudia timu ya Jamhuri wakiumana na Timu iliyopanda Daraja Msimu huu, Timu ya Kizimbani.

Kwa upande wa Kisiwa cha Unguja itashuhudia pambano kati ya Malindi na Polisi pambano litakalopigwa katika Uwanja wa Mao Tse Tung.

No comments:

Post a Comment