BUKOBA SPORTS

Monday, November 4, 2013

CRISTIANO RONALDO AKIFUKUZIA KWA KARIBU KIATU CHA DHAHABU ULAYA.

NYOTA wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo anakijongea kwa karibu kiatu cha dhahabu cha Ulaya kufuatia kiwango bora alichoonesha uwanjani katika siku saba zilzioita. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno aliiga mabao matatu katika ushindi wa Madrid wa mabao 7-3 dhidi ya Sevilla katikati ya wiki huku akitupia mengine mawili katika mchezo walioshinda mabao 3-2 dhidi ya Rayo Vallecano. Hata hivyo kazi hiyo haitakuwa rahisi kwa Ronaldo kwani anafuatiwa kwa karibu na nyota wa Atletico Madrid Diego Costa waliyetofautiana kwa alama moja. Majina mengine makubwa yaliyoingia katika kumi bora ni amoja na Robert Lewandoski, Giuseppe Rossi na Edinson Cavani amba wote wana alama 18.Real Madrid walipoifunga Rayo juzi bao 3-2. na hapa walikuwa wanashangilia baadhi ya bao walilofunga!

No comments:

Post a Comment