Bao la Dakika ya 89 kwa kichwa cha Daniel Sturridge alietokea Benchi limewanusuru Liverpool na kupata Sare ya Bao 3-3 walipocheza Goodison Park na Mahasimu wao wakubwa katika Dabi ya Merseyside.
Mara mbili Liverpool waliongoza na mara
mbili Everton wakarudisha na hatimae Romelu Lukaku kuifungia Everton Bao
la 3 katika Dakika ya 82 na kuwapa matumani ya ushindi lakini Sturridge
akasawazisha kwa kichwa baada ya frikiki.
Sare hii imewabakisha Liverpool Nafasi ya Pili sasa wakiwa Pointi 1
nyuma ya Arsenal lakini wao wamecheza Mechi moja zaidi na kuwapandisha
Everton hadi Nafasi ya 5.
Coutinho akishangilia kwa aina yake baada ya kufunga bao katika dakika ya 5 kwenye uwanja wa Goodison Park leo jumamosi kwenye ligi kuu.
Coutinho akipongezwa na wenzie!
Kevin Mirallas kwenye patashika na Steven Gerrard
Mchezaji wa Everton Mirallas akishangilia baada ya kufunga bao dakika ya 8
Luis Suarezakiachia friikiki dakika ya 19 na kufunga goli.
VIKOSI:
EVERTON (4-3-3): Howard 8:
Coleman 7, Jagielka 8, Distin 7, Baines 7 (Deulofeu 50mins 7): Barry 8,
McCarthy 7, Pienaar 7: Barkley 8, Lukaku 9, Mirallas 8 (Osman 88).Subs not used: Robles (GK), Heitinga, Jelavic, Deulofeu, Naismith, Osman, Stones
Booked: Distin, Miralles, Barkley
Scorers: Miralles 8', Lukaku 72', 82'
LIVERPOOL (4-1-3-2): Mignolet 8: Johnson 6, Skrtel 7, Agger 6, Flanagan 7: Lucas 8 (Sturridge 79mins): Gerrard 8, Allen 5 (Moses 67mins 6), Henderson 8; Coutinho 6: Suarez 7
Subs not used: Jones (GK), Toure, Luis Alberto, Sakho, Sterling
Booked: Lucas, Allen, Suarez
Scorers: Coutinho 5', Suarez 19', Sturridge 89'
No comments:
Post a Comment