Chelsea na Manchester City leo zimeshinda Mechi zao za Ligi Kuu England walizocheza Nyumbani na kuikaribia Arsenal ambao wapo kileleni na pia kuishusha Liverpool iliyokuwa Nafasi ya Pili na kuitupa Nafasi ya 4.
Wakati Liverpool hii leo ikichapwa Bao 3-1 na Hull City, Chelsea ilishinda kwake Stamford Bridge kwa kutoka nyuma kwa Bao 1-0 hadi Haftaimu na kuifunga Southampton Bao 3-1.
Bao za Chelsea zilifungwa na Gary Cahill, John Terry na Demba Ba, alieingizwa Kipindi cha Pili.
Bao la Southampton, lililofungwa katika Dakika ya Kwanza tu, lilipachikwa na Rodriguez.
Huko Etihad, Bao la Negredo na mbili za Samir Nasri, ziliwapa Manchester City ushindi wa Bao 3-0 walipoichapa Swansea City.
Ushindi wa leo umeifanya Chelsea ikamate Nafasi ya Pili ikiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Arsenal na Nafasi ya Tatu imeshikwa na Man City walio Nafasi ya Tatu na wapo Pointi 2 nyuma ya Chelsea.
Jay Rodriguez ndie alieanza kuifunga Chelsea na kuipatia bao timu yake

Pongezi za aina yake hapa!!

Wachezaji wa Chelsea hoi!

John Terry kunani hapa!!

Rodriguez akichuana na Ivanovic wa Chelsea kushoto nyuma.,.

Oscar kiatu kilimpitia ...chini akijiuguza

Majanga!!

Victor Wanyama na Juan Mata wakigombea kutwaa mpira hapa!

Branislav akigonga mpira kwa kichwa

Demba Ba akitupia

Ivanovic na Cahillwakipongezana baada ya kupata bao

Capten John Terry akifana 2-1

Pamoja na kufunga bao hilo la pili Jose Mourinho bado alikuwa anahitaja mabao mengine zaidi

Demba Ba akisindikiza mpira nyavuni na kufunga bao la ushindi dhidi ya Southampton usiku huu

Furaha ya Ushindi: Ramires, Demba Ba na wakiponezana na kupeana tano!!
No comments:
Post a Comment