BUKOBA SPORTS

Sunday, December 1, 2013

DKT.BILAL AENDESHA ZOEZI LA HARAMBEE YA KUCHANGIA MADAWATI MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU JIMBO LA NKENGE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi chaeti, Mkurugeniz wa Kagera Sugar, Bw. Hamadi Yahaya, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuchangia maendeleo ya Elimu ya Jimbo la Nkenge mkoa wa Kagera,wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali (mst) Fabian Masawe. Jumla ya Shilingi milioni 114, pesa taslimu milioni 65.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe.

Sehemu ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo

Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo

Meza Kuu wakijumuika kuimba wimbo maalumu wa mkoa wa Kagera wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo, hususan katika suala la elimu na kuchangia madawati.

Msanii Saida Karoli na kundi lake wakiburudisha wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Picha na OMR.

No comments:

Post a Comment