Mmiliki wa Hull Assem Allam anaetaka kubadili jina na kuwa Hull Tigers
Hull City wameomba rasmi kwa FA, Chama cha Soka England, kubadili Jina lao na kuwa Hull Tigers kuanzia Msimu ujao. Mmiliki wa Klabu hiyo, Assem Allam, anataka kubadili Jina hilo ili kuvutia Soko lake Kimataifa na Mwezi Agosti alibadili Jina la Kampuni ya Biashara inayoiendesha Klabu ya Hull City na kuwa Hull City Tigers.
Mabadiliko haya yamezua upinzani mkubwa toka kwa Mashabiki wa Hull City ambao wameanzisha Kikundi cha kupinga hatua hiyo kiitwacho "City Till We Die" ambacho kinadai mabadiliko hayo ni kuitupa Historia ya Klabu hiyo.
HISTORIA:
-Ilianzishwa Mwaka 1904.
-Walivaa Jezi za Jeusi na Njano kwa Msimu wao wa Kwanza.
-Walibatizwa Jina la Utani 'Tigers' Mwaka 1905 na Mwandishi wa Gazeti la Hull Daily Mail.
-Baada kutumia Uwanja wa Boothferry Park kwa Miaka 56, walihamia KC Stadium Mwaka 2002.
Kiutaratibu, mabadiliko yeyote ya Jina la Timu ni lazima yapitishwe na Baraza la FA na huanza kutumika Msimu unaofuata.
Mmiliki wa Hull City, Assem Allam,
mwenye Miaka 74, ni Mzaliwa wa Egypt, ambae alihamia Mji wa Hull Mwaka
1968 na kuanza kuimiliki Hull City Desemba 2010 na kuinusuru kutoka
kufilisiwa na pia kuipandisha Ligi Kuu England Msimu huu, hii ikiwa ni
mara yao ya pili kucheza Ligi Kuu katika Historia yao ya Miaka 109.
Kubadilishwa kwa Jina la Klabu kumeleta
msuguano ambapo Allam alikaririwa akiwaambia Mashabiki wanaopinga hatua
hiyo ‘wanaweza kufa kwa wakati wao’ kitu ambacho Meneja wa Timu hiyo,
Steve Bruce, alisema kilikaririwa vibaya.
No comments:
Post a Comment