KIUNGO mahiri wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amekubali adhabu aliyopewa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA lakini atapinga adhabu ya kufungiwa mechi mbili aliyopewa. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza alikuwa akituhumiwa kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wa Manchester City katika uwanja wa Etihad baada ya timu yake kupewa kipigo cha mabao 6-3 katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika wiki iliyopita. Tukio
hilo halikuonwa na mwamuzi wa mchezo huo lakini picha za video
zilimuonyesha Wilshere akitoa ishara hiyo na FA kumpatia adhabu kwa
sheria mpya ambayo huwaruhusu kufanya hivyo kama tukio halikuonekana na
mwamuzi. Kesi yake inatarajiwa kusikilizwa Alhamisi na kama adhabu
ikibaki hivyo nyota huyo anatarajiwa kukosa mechi mbili za Ligi Kuu
ukiwem mchezo dhidi ya Chelsea Desemba 23 na mchezo dhidi ya West Ham
United siku tatu baadae.Jack Wilshere alivua jezi baada ya kibano cha bao 6-3 kutoka kwa City.
No comments:
Post a Comment